Thursday, September 9, 2010

Kitchen Party

Design bomba...


Katika hii shughuli nimependa sana design ya nguo zao, usipokuwa makini unaweza kufikiria wamevaa sare lakini kuna some little details ambazo zipo kwenye ngua ya Bi Harusi mtarajiwa zinamiss kwenye nguo ya matron wake.
Watu wengi wamekuwa na wasiwasi sana wa kuvaa nguo za kufanana hasa kwenye shughuli zao kama vile Kitchen Party, sendoff na Harusi... but take it from me Bibi harusi siku zote ana nafasi yake kwenye shughuli yake so hata mkiamua kuvaa sare but bibi Harusi atakuwa mmoja tu...


Kitu kingine muhimu ni maombi...
Ni shughuli chache sana utakuta wanamuweka bi harusi kati na kuanza kumuombea kama muonavyo pichani...
Si kila mtu anakuja kwa nia njema kwenye sherehe kama hizi, na hukawii kusikia Bi Harusi baada ya kutoka ukumbini kaumwa nusu ya kufa halafu ugonjwa hauonekani. Kumbe kama maombi au dua ingefanyika ingeweza kuepusha mengi.
Kwa imani yangu wanandoa au maharusi wengi wanashauriwa hata kuombea zawadi zao kabla ya kuzifungua, ili kuvunja laana, maagano au chochote kilichonenewa juu ya zawadi hizo kisiwadhuru.

Kwa sasa ni hayo tu... mengi zaidi yanakuja
Asante Shamim wa 8020 kwa picha

1 comment:

Total Pageviews